Sunday, August 26, 2018

Serengeti boys wa tatu Uganda ikitwaa ubingwa mbele ya raisi wa CAFTimu ya vijana ya Uganda iliyoitoa Serengeti boys ya Tanzania imeibuka mabingwa wa mashindano ya CECAFA chini ya miaka 17 baada ya kuwachapa vijana wa Ethiopia magoli 3-1.

Mbele ya rais wa shirikisho la soka Afrika CAF  Ahmad Ahmad  Kikosi cha Uganda kimemaliza mashindano ya CECAFA kwa kuonyesha soka safi na walionyesha wamekoma vilivyo katika soka.

Mabao ya  ushindi ya Uganda yamefungwa na Kasozi Samson dakika ya 14 na Abdulwahid Iddi, mawili dakika za 61 na 85 ya mchezo huo.

Kwa matokeo hayo sasa vijana wa Uganda chini ya umri wa miaka 17 wamekata tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON kwa vijana wa umri huo hapa nyumbani Tanzania kuanzia May 12.

Katika mchezo mwingine wa kumtafuta mshindi wa tatu timu mwenyeji Serengeti boys ya Tanzania imeibuka na nafasi hiyo kwa mabao 4-3 kwa njia ya matuta baada ya dk 90 kumalizika kwa sare ya magoli 2-2.

SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: