Sunday, August 26, 2018

Samatta afunga tena baada ya kufunga hat trick wiki iliyopita.
Baada ya kufunga magoli matatu yaani hat trick kwenye ushindi wa 5-2 dhidi Bondby katika Play off ya Europa League Mbwana Ally Samatta ameendeleza kasi yake ya kufumania nyavu baada ya hapo jana kuifungia tena klabu yake ya KRC Genk.

Hapo jana Samatta amefunga goli moja katika ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Waasland Beveren akiingia dk ya 59 na dakika ya 78 akaisawazishia Genk bao baada ya Beveren kufunga bao la pili katika dakika ya 66.

Beveren walijifunga dk 89 kupitia kwa beki wao Maximiliano na kuwapatia Ushindi Genk katika mchezo huo wa First Divission A kule Belgium.

Samatta amekuwa kwenye kiwango kizuri saana msimu huu na amekuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo waliompachika majina mengi kutokana na kuzifumania nyavu mara kwa mara.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: