Saturday, August 18, 2018

Ronaldo ashindwa kufunga mechi ya kwanza messi, Mbappe ni habari nyingineMshambuliaji bora duniani Cristiano Ronaldo jana amecheza mchezo wake wa kwanza wa ligi ya italia dhidi ya Chievo Verona  akiwa na kikosi cha Juventus ambapo amehamia huko akitokea Real Madrid ya Hispania.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Juventus kushinda magoli3-2  Ronaldo hakufunga goli lolote kama wengi walivyotarajia wakiamini pengine angefunga katika mchezo wa jana.

Magoli ya ushindi ya  juventus yamefungwa na Khedira dk 3, Bonucci na  Bernardeschi akijifunga dk 90 huku magoli mawili ya Chievo Verona yakifungwa na Stepinski dk 38, Giaccherini kwa penalti dk 56.

Wakati Ronaldo akishindwa kufunga mpinzani wake Lioneli Messi amefunga magoli mawili timu yake ya FC Barcelona ikishinda magoli 3-0 katika mchezo wao wa kwanza wa laliga dhidi ya Deportivo Alaves nyumbani.

Messi amefunga magoli hayo dk ya 64 na 90 huku goli jingine likifungwa na coutinho dk 83 mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Jose Maria Sanchez Martinez raia wa Hispania.

Kule nchini Ufaransa PSG imeshinda 3-1 dhidi ya Guingamp katika mchezo wa kwanza mchezo ambao Kylian Mbappe aliingia dk ya 46 kipindi cha pili na kufunga magoli mawili dk ya 82 na 90 huku Neymar akifunga goli la kwanza dk ya 53 kwa mkwaju wa penati.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: