Tuesday, August 21, 2018

Rock city derby kupigwa hapo kesho ccm kirumba sasa ni tumbo joto kila upandeTambo za Mechi Kubwa Jijini Mwanza ambayo inafahamika kama Rocky City Derby baina ya Alliance Fc kutoka Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza wakichuana na Mbao Fc wakitokea Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. 

Mengi yamesemwa Kuelekea mechi hiyo ila dakika tisini za Mwamuzi wa katikati ndizo zitaamua nani ataibuka na pointi katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu baina ya timu kutoka Mkoani Mwanza.

Mashabiki na wapenzi wa timu hizo Wamezungumza mengi Ila ukweli mchezo huo unatabiriwa kuwa mgumu kutoka na uimara wa timu hizo mbili Alliance na Mbao. Mbao wana uzoefu wa ligi Kuu wakicheza Msimu miwili na huu unaonza unakuwa wa tatu ila Alliance wao ndio Msimu wa Kwanza. 

Mchezo huo wa kwanza wenyeji Watakuwa Alliance Fc kutoka kata ya Mahina Wilaya ya Nyamagana. Kocha Msaidizi wa timu hiyo Kessy Mziray amesema kuwa wanawaheshimu Mbao Sana Ila watacheza kwa mbinu umakini na kuzingatia mipango yao ya mechi hiyo ili waibuke na Ushindi.

Kwa Upande wa Kocha Mkuu wa timu ya Mbao Amri Said maarufu kama Stam, amesema amewaandaa vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo ingawa utakuwa mchezo mgumu kulingana na hamasa ya Wanamwanza na Mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa. 

Nahodha wa timu ya Alliance Fc Hance Masoud na Nahodha wa timu Mbao Fc David Mwasa wote wamesema ushindi kila upande ni Kitu cha kwanza katika Mechi hiyo Kubwa Jijini Mwanza ikizikutanisha timu hasimu za kutoka Mkoani hapo. 

Ukiangalia vikosi vyote vya timu hizo Alliance Fc wana robo tatu ya Kikosi kilichoipandisha timu hiyo ligi Kuu hivyo wamekaa pamoja Muda mrefu tofauti na Mbao Fc ambao wachezaji wake Wengi wamesajiliwa timu tofauti na kumpa nafasi Kocha Amri Said kasajili wachezaji wengine.

Kijogragia na upepo mkubwa wa watu wa Mwanza ni kama wanaipa nafasi Kubwa Alliance Fc ingawa ubashiri huo unaweza kubadilishwa na matokeo yatakayopatikana dakika tisini na wakichagizwa na mbinu za makocha kimchezo.

Boniface Mathias Nduha ni Mdau wa Soka Mkoani Mwanza anasema kuwa "Mbao wanakufa Mapema Sanaa maana Alliance ni timu hatari Sana" . "Uwezekaji Mkubwa uliofanywa na Menejimenti ya timu hiyo sio wa kubezwa kabisa ".

Shabiki wa Mbao Fc John Maseto kutoka Buswelu wilaya ya Ilemela amesema kuwa "Alliance ni timu ya Wanafunzi hivyo haina mbinu za kuwavuia kafungwa na Mbao " Sisi hatusomi, tunaranda Mbao hiyo watarandwa uwanjani wapendeze" alisema. 

Utofauti wa timu hizo ni 
Wako wilaya tofauti, Alliance wakitokea Wilaya ya Nyamagana na Mbao wakitokea wilaya ya Ilemela. Wako majimboni tofauti, Alliance wako Jimbo la Nyamagana ambalo Mbunge ni Mheshimiwa Stanslaus Mabula na Mbao wako Jimbo la Ilemela wakiongozwa na Mbunge Daktari Angelina Mabula. Wako Halmashauri tofauti, Alliance wako Halmashauri ya Jiji la Mwanza, na Mbao wako Halmashauri ya Manisapaa Ilemela... 

22/8/2018 ndio Watu watajua nani atakuwa mbabe Kwa Mwenzake, ama Alliance Fc wenyeji wa mchezo Kuibuka washindi ama Mbao Fc kutumia uzoefu wao kuibuka na Ushindi wa mechi hiyo muhimu itakayotoa picha kamili maandalizi yao na Ubora wa Kikosi kwa Michuano ya Ligi Kuu na Mashindano Mengine yanayosimamiwa na TFF. 


Timu hizo mbili zinadhaminiwa na Kampuni kubwa na maarufu iitwayo GF Trucks & Equipments ambayo inasambaza vifaa vya migodini. Meneja Masoko wa GF Kulwa Bundala anasema " Sisi GF timu hizi ni zetu kazi inabaki kwa kila timu Wakiongozwa na mabenchi yao ya ufundi kutimiza majukumu yao pamoja na wachezaji Kuibuka na ushindi" alisema.SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: