Sunday, August 26, 2018

Rais wa CAF yupo nchini kutazama mtanange wa fainali ya vijana chini ya miaka 17 leoRais wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad atashuhudia mchezo wa  fainali ya CECAFA kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazo fanyika leo katika uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na mtandao rasmi wa CAF zinasema Rais huyo atakuwa miongoni mwa watakao shuhudi mchezo utakaozihusisha timu za Uganda na Ethiopia utakaoanza saa 11 jioni.
Kabla ya mchezo huo wa Fainali kutakuwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa baina ya Tanzania dhidi ya Rwanda utakaonza saa 8 alasiri.
Mshindi wa mchezo wa fainali ataungana na wenyeji Tanzania kuwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na kati katika michuano hiyo itakayoanza may 12 mwakani.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa na Azam Complex, Chamazi.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: