Saturday, August 25, 2018

PSG ni mwendo wa dozi tu huko nchini UfaransaWashambuliaji Edison Cavani, Kylian Mbappe na Neymar wamefunga kila mmoja wakati Paris Saint German ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Angers katika ligi kuu nchini Ufaransa.
Washambuliaji hao waliunda safu hatari ya ushambiliaji msimu uliopita na kuiwezeha PSG kutwaa ubingwa wa Ligue 1.
Dk ya 12 Cavani alitangulia kuipatia timu yake goli kabla ya Mbappe kufunga goli la pili dk ya 51 baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Angel Di Maria huku goli la tatu na la ushindi likitiwa kimiani na Neymar dk ya 66 baada ya kupokea pasi ya Mbappe.
Goli pekee na la kufuatia machozi la Angers limefungwa na Thomas Mangani kwa mkwaju wa penati dakika ya 22.
PSG ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu mpaka sasa.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: