Thursday, August 16, 2018

POGBA atimuliwa kucheza soka sababu ya uzito uliopitiliza


Baada ya kukosa timu ya kuchezea kwa mwaka mmoja hivi sasa kaka yake kiungo wa Manchester United, Paul Pogba anayeitwa Mathias Pogba ameshindwa kuitumikia timu moja huko nchini ujerumani kwa kuwa na uzito uliopitiliza.

Mathias Pogba mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni kaka mkubwa wa Paul Pogba ameshindwa kujiunga na klabu ya KFC Uerdingen ya nchini Ujerumani baada ya kufeli majaribio kutokana na kuwa na mwili mkubwa unaochangia kumjengea kuwa na hips na ongezeko la kilo.


Alipohojiwa kuhusu kushindwa kujiunga na KFC Uerdingen Meneja wa klabu hiyo, Stefan Kramer amesema Pogba tayari ameshaondoka baada ya kufeli majaribio.

 Mathias Pogba mwenye umbile kubwa la futi 6 anayeitumikia timu ya taifa ya Guinea kwa sasa ni mchezaji huru toka kuacha kuitumikia klabu ya Sparta Rotterdam mwaka 2017 hana timu.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: