Thursday, August 23, 2018

Nusu fainali za CECAFA chini ya umri wa miaka 17 kupigwa hapo keshoMichuano ya CECAFA kwa umri chini ya miaka 17 kuwania kufuzu michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri huo inatarajia kuendelea hapo kesho  hatua ya nusu fainali.

Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 serengeti boys watacheza dhidi ya vijana wa Uganda saa kumi na mbili kamili jioni.

Nusu fainali nyingine itafanyika mapema saa nane kamili mchana ambapo Ethiopia watacheza na Rwanda .

Bingwa wa michuano hii ataifuzu moja kwa moja kucheza michuano ya AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika mwakani hapa nchini.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: