Sunday, August 19, 2018

Nilichokiona Mechi ya Ngao ya Jamii baina Simba na Mtibwa CCM Kirumba .


Fabian Fanuel @FMG
Mwanza
Sehemu ya Kwanza

ILIKUWA siku ya furaha nderemo na vifijo kutoka na jiji la Mwanza kupata wageni wengi kutoka mikoa mbalimbali kuja kushuhudia mechi ya Ngao ya Hisani ya timu ya Simba Sc Mabingwa wa Kombe la Ligi na Mtibwa Sugar mabingwa wa Kombe la Azam Sports Federation katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Maandalizi ya Mechi hii yalianza tu pale ambapo kamati ya utendaji ya shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF kwa ushirikiano mzuri ya bodi ya ligi kuupa Mkoa wa Mwanza heshima ya kufanyika mechi hii kubwa ya ngao ya hisani ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nje ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo huwa inafanyika mara kwa mara toka ianzishwe.

Kadri siku zilipokuwa zinasogea kuelekea mechi hiyo, hamasa kubwa ilizidi kuongezeka kwa wapenzi  na mashabiki wa timu ya Simba na Mtibwa pamoja na mashabiki wa timu pinzani wengine wakiiunga simba mkono na wengine wakiiunga Mtibwa mkono wa kushinda hiyo mechi ya ngao ya hisani.

Utamu wa Mechi hiyo uliongezwa na maandalizi thabithi ya Simba nchini uturuki na Mtibwa ambao walikuwa nchini kujiwinda na mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ambayo inatarajia kuanzia jumatano tarehe ishirini na mbili mwezi agosti mwaka elfu mbili kumi na nane.

Nini Kilifuata, Itaendelea kesho.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: