Thursday, August 23, 2018

Nilichokiona Mechi ya Ngao ya Hisani Simba na Mtibwa Uwanja wa CCM KIRUMBA.

Fabian Fanuel @FMG 
MWANZA

SEHEMU YA TATU

Baada ya Simba Day kukamalika Simba walienda Lindi kucheza na Namungo Fc wakatoka sare, Kisha wakaenda Arusha kucheza na Arusha Uniteda wakatoka sare kisha wakaja Mwanza kujiwinda na mechi ya Ngao ya Hisani didhi ya Mtibwa Sugar uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Simba alifika Mwanza  Ijumaa asubuhi tarehe kumi na saba agosti na Mtibwa wakifika Mwanza Alhamis Usiku wakitokea Manungu Turiani Morogoro.

Baada Mtibwa kufika Mwanza walifanya mazoezi Ijumaa asubuhi katika Uwanja wa CCM Kirumba na baadae mchana kukawepo press conference na waandishi wa habari iliyoandaliwa na TFF ili Mabenchi ya ufundi kwa timu zote yazungumzie mechi itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila na Nahodha wa timu hiyo Shaban Nditti walisema wao hawaogopi mechi yao na Simba hata kama walikuwa Uturuki, wanaamini wana kikosi kizuri na wamejiandaa kupambana hadi dakika tisini na lengo lao ni kuibuka na Ushindi wa Ngao ya hisani ili kuweka rekodi mpya hapa Tanzania.

Kocha Patrick Aussems na Nahodha wa timu hiyo John Bocco wao walitanabaisha kuwa hawana mchezo na mechi hiyo maana wanakikosi kipana na wana majeruhi wawili tuu ila timu nzima iko vizuri na wanaamini watawapa raha mashabiki na wapenzi wao wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla. Baada ya Mkutano na waandishi wa habari Simba jioni wakawa na mazoezi ya kujiweka sawa katika uwanja wa Nyamagana.

Nini Kilifuata, itakuja hapa kesho.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: