Sunday, August 19, 2018

Makala-Nilichokiona Mechi ya Ngao ya Hisani Simba na Mtibwa CCM Kirumba.

Fabian Fanuel @FMG
MWANZA

Sehemu ya Pili.

Simba alijichimbia nchini Uturuki kwa mazoezi ya kujiandaa na Mtibwa alibaki nyumbani akiweka kambi yake hapo. Kutokana na usajili wa Simba ilioufanya na wachezaji iliyobaki nao msimu uliopita hadi kuchukua kombe la ligi kila mtu aliamini Simba itakuwa moto wa kuotea mbali kwa sababu ya kuwa na wachezaji wazuri na kuwa na uongozi imara chini ya kaimu Rais Salim Abdalla huku mwekezaji Mohamed Dewji akichagiza kuweka mpunga wa kutosha kuendesha timu hiyo.

Simba akiwa Uturuki alicheza mechi mbili na kutoka sare moja na kushinda moja. Kitendo ambacho kilianza kuwapa hamasa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuwa mechi ya ngao ya hisani Simba itawapa raha kubwa sana. Simba walirejea katika adhi ya Tanzania kwa ajili ya kujiandaa na Simba Day ambapo ni siku maalum kwao ya kutambulisha kikosi chao kipya, kumtambulisha jezi na kutambulisha benchi la ufundi kwa msimu mpya wa ligi unaoanza.

Siku ya Simba Day ilifika ambayo ni tarehe nane mwezi wa nane kila mwaka ambapo Simba huwa wanifanyia katika himaya yao jijini Dar es Salaam, na kwa mwaka huu waliialika timu nguvu Africa kutoka nchini Ghana iitwayo Asante Kotoko. Siku ya tukio baada ya kufanya utambulisho wao na ilifuata mechi hiyo kati ya Simba na Asante Kotoko ambapo awali ilitanguliwa na mechi ya Simba Queens na Under 20 ya Simba ambao walicheza na Dodoma Fc.

Katika Mechi hiyo Simba alifungana goli moja kwa moja na Asante Kotoko na kuifanya mechi kumalizika kwa matokeo hayo ya sare. Baada ya mechi hiyo kukamilika ambapo mashabiki wengu wa timu ya Simba walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa wakiwa wamevaa sare zao nyekundu na nyeupe wakiufanya Uwanja wote uwake kwa rangi mwanana nyekundu na nyeupe. Baada ya Kukamilika kwa mechi hiyo hemwa hemwa ikawa kujipanga na mechi ya ngao ya hisani.

Itaendelea Kesho sehemu ya tatu

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: