Friday, August 31, 2018

MOROGORO | Mwigulu Nchemba kuwa mgeni rasmi tamasha kubwa Mkoani Morogoro Jumapili hii, usikose tafadhali.

Fabian Fanuel @FMG

Mbunge wa Iramba Mashariki kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mwigulu Lameck Nchemba anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha kubwa la uzinduzi wa albam iitwayo MUNGU  ANAONEKANA yake mwimbaji mkongwe wa siku nyingi TUMAINI NJOLE SEHEBA.

Akizungumza na Blog ya Famara News, Mratibu wa tamasha hilo Tumaini Njole alisema maandalizi yamekamilika kuelekea tukio hilo kubwa ambalo limesubiriwa kwa hamu na muda mrefu na wapenzi wa muziki wa injili ambao wanamsapoti mwimbaji huyo.

''Maandalizi yanaendelea vizuri na hadi sasa kila kitu kinaelekea kukamilika maana Uwanja wa Jamhuri tayari tumepewa na wahusika, pia waimbaji kutoka mikoa mbalimbali wamethibitisha kuja kushiriki baraka hizi, na kikubwa Mgeni Rasmi Mbunge Mwigulu Nchemba naye yuko tayari kwa kazi hii kubwa'' alisema Njole.

Tamasha hilo kubwa la uzinduzi wa albam na kusherehekea miaka kumi na tano ya huduma yake Tumaini Njole  utafanyika Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri ambapo waimbaji wengi watashiriki kuimba, watumishi wa Mungu pia kutoka madhehebu mbalimbali watakuwepo.

Ametaja kiingilo kuwa ni wakubw kuwa ni elfu mbili huku watoto wakitoa elfu moja ili kusapoti huduma hiyo ambayo imekuwa baraka kwa watu wengi nchini Tanzania na nje ya mipaka.

Famara Media Group inamtakia mafanikio mema katika tukio hilo la kihistoria na kumwomba akimaliza huko aje na Mwanza kuwapa wapenzi wake raha ya albam yake ya Video.

Pata nafasi ya kutazama wimbo wake wa Video hapa chini.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: