Thursday, August 30, 2018

Modric,Ramos,CR7 watwaa tuzo michuano ya ulaya
Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Croatia Luka Modric amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya akiwapiki Mohamed  Salah pamoja na Cr7 wa Juventus.
Luka Modric, ametwaa tuzo ya kiungo bora wa mashindano ya uefa msimu wa mwaka 2017/18 baada ya kuisaidia timu yake ya madrid kutwaa taji la Ligi ya mabingwa.
Kyle Navas, ambaye nae ni wa Real Madrid ametwaa tuzo ya goli kipa bora wa michuano ya uefa msimu wa mwaka 2017/18.
Cristiano Ronaldo ambaye sasa yupo juventus ya italia, ametwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa michuano ya Uefa msimu wa mwaka 2017/18 wakati akiitumikia klabu yake ya zamani ya Real Madrid
Bechkam pia amepokea tuzo ya heshima kutoka uefa kutokana na mchango wako mkubwa katika soka

Sergio Ramos,amewapiku mabeki wenzake wa Madrid Varane na Marcelo na  kutwaa tuzo ya beki bora kwenye michuano ya uefa msimu wa mwaka 2017/18.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: