Thursday, August 23, 2018

VIDEO-Mnyama simba anguruma,Alliance yachapwa matokeo na ratiba ya TPL hii hapa
Ligi kuu ya  soka Tanzania bara TPL kwa msimu wa mwaka 2018-2019  imeanza kutimua vumbi hapo jana kwa michezo sita kupigwa kunako viwanja sita tofauti nchini.

Mbali na mchezo wa Rock city derby ama GF derby kama sio SATO derby ambao mbao wamewafundisha soka wadogo zao Alliance kwa kuwachapa Goli 1-0 uwanja wa CCM Kirumba mwanza mchezo mwingine mkubwa Simba ilishinda 1-0 pia dhidi ya Prisons goli pekee la Meddie Kagere dk ya 2 ya mchezo.

Matokeo mengine  ya michezo ya jana KPL  Ndanda FC wameshinda ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na wakamua alizeti Singida United wamefungwa 1-0 nyumbani Uwanja wa Namfua na Biashara.

Kagera Sugar imeanza vizuri kwa ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Coastal Union, timu kipenzi cha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imelazimishwa sare ya 1-1 Lipuli FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Ligi hiyo itaendelea leo,kwa michezo kadhaa Yanga SC dhidi ya  Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Saa 12:00 jioni, JKT Tanzania wakijiuliza dhidi ya KMC mapema  kuanzia Saa 8:00 mchana Uwanja wa Meja Isamuhuyo, Stand United na African Lyon Saa 10:00 Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Azam FC na Mbeya City kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.


GOLI LA MEDDIE KAGERE HILI HAPA TAZAMASHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: