Tuesday, August 28, 2018

Miradi ya mabilioni kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga Mhe. Zainab Telack kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Izizimba A wilayani Kwimba.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella juzi Agosti 26, 2018 amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea mkoani Shinyanga.

Akizungumza kwenye mapokezi hayo yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Izizimba A wilayani Kwimba, Mhe.Mongella alibainisha kwamba mwenge huo unatarajia kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 13.

Naye kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ndugu Charles Kabeho alimpongeza Mhe.Mongella kwa mapokezi makubwa na kuahidi kukagua miradi yote iliyokusudiwa hatua kwa hatua ili kujiridhisha ubora wa utekelezaji wake.

Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza zinatarajiwa kufikia tamati jumapili ijayo Septemba 02,2018 na kukabidhiwa mkoani Mara jumatatu Septemba 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa Mwanza akipokea mwenge wa Uhuru
Tazama picha mbalimbali za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza
Tazama BMG Online Tv hapa chini

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: