Thursday, August 23, 2018

Mechi ya Mnyama Simba dhidi ya Mbeya City yahairishwa sio kesho tena kupigwa jumatatu...
Mchezo wa ligi kuu kati ya timu ya mabingwa wa ngao ya hisani Simba dhidi ya Mbeya City uliopangwa kufanyika siku ya kesho Jumamosi katika uwanja wa Taifa sasa utafanyika Jumatatu saa 12 jioni.

Mabadiliko hayo yametokana na kupisha maandalizi ya mechi ya fainali ya michuano ya kufuzu fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 itakayopigwa uwanjani hapo Jumapili, Agosti 26.
Michuano hiyo ya vijana imeingia nusu fainali ambapo kesho Rwanda itacheza na Ethiopia saa nane mchana huku wenyeji Tanzania timu ya Serengeti boys wakicheza na Uganda saa kumi na moja jioni mechi zote zikipigwa kesho uwanja wa Taifa.
Mkurugenzi wa bodi ya ligi, Boniface Wambura ndiye aliyetangaza mabadiliko hayo muda mfupi uliopita.
Mbali na mabadiliko hayo mchezo mwingine kati ya Azam FC dhidi ya Ndanda utapigwa saa 2 usiku siku ya Jumatatu badala ya saa 1 ya awali.
Simba imeshinda mchezo wake wa kwanza goli 1-0 dhidi ya Prisons ya mbeya wakati Vinara wa ligi hii ya TPL Azam wakishinda 2-0 dhidi ya Mbeya city pia kutoka mbeya


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: