Monday, August 27, 2018

Man united hali yao sio nzuri yapata kipigo cha 3 mzuka dhidi ya TottenhamTimu ya mashetani wekundu Manchester united usiku wa jana imeambulia kichapo kitakatifu cha magoli 3-0 dhidi ya timu ambayo haikufanya usajili Tottenham Hospurs katika uwanja wa Old Trafford.
Ushindi huo wa kwanza kwa Tottenham Hospurs baada ya miaka minne katika uwanja wa Old Trafford umewafanya pia Tottenham kuungana na Liverpool,Chelsea na Watford kuwa timu pekee zilizoshinda michezo yake mitatu hadi sasa.
Huu ni ushindi wa kwanza wa kocha Mauricio Potchetino katika uwanja huo tangu aanze kuifundisha Spurs ambapo walikuwa hawajawahi kupata bao katika uwanja huo.
Magoli ya washindi yamefungwa Harry Kane aliyefunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 49 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na mlinzi Kieran Trippier.
Dakika ya 51, Lucas Maura aliifungia Spurs bao la pili baada ya kupokea pasi ya Christian Eriksen kufuatia shambulizi la kushtukiza.
Moura alipigilia msumari wa mwisho katika jeneza la United baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 85.
Kipigo hicho kitakatifu kwa united walioshinda mchezo mmoja tu hadi sasa dhidi ya Leicestercity kimeweka rehani kibarua cha Jose Mourinho huku akionekana muda wake ukiwa umefikia tamati punde.
SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: