Sunday, August 19, 2018

Makala Part 3 - Moshi mweusi waendelea kufukuta ndani ya timu ya Toto AfricansFabian Fanuel @FMG
MWANZA

Sehemu ya Tatu
Msimu wa 2016 klabu ya Toto Africans walishiriki ligi kuu baada ya kukwepa kushuka daraja na nguvu yao ikaendelea kudorora kutoka na baadhi ya Wanachama kutokuwa na Elimu ya kutosha kuhusu uwekezaji ndani ya klabu na sio kutegemea mapato ya klabu ndio wajilipe kutoka na kazi wanayoifanya ndani ya timu hiyo.

Mwenyekiti wa timu hiyo Godwin Aiko na Makamu Mwenyekiti ni kama hawakuwa wanaiva kutokana na kila mmoja kuwa na wajumbe wa wanachama wanaomuunga mkono, kitu ambacho kiliendelea kuiyumbisha timu hiyo wakati haikuwa na mdhamini zaidi ya kutegemea jengo lao liliko mtaa wa Kishamapanda na wadau wachache kuisapoti timu kusafiri na kulea timu hiyo.

Matokeo ya Uwanja ya timu yaliianza kuwa mabaya hatimaye kocha aliyekuwa anakaimu nafasi ya kocha Mkuu Rogasian Kaijage kujiweka pembeni na timu ikaendelea kuwa yatima ingawa Kocha Khalfan Ngassa aliendelea kukaimu majukumu hayo ya ukocha ila akaja kuwekwa nje na kanuni za TFF kuwa hana leseni inayotosheleza mahitaji ya nafasi ya ukocha mkuu.

Hatimaye kamati ya utendaji wakamtafuta kocha mwingine ambaye angekuja kuinusuru na janga la kufunga nyumbani na ugenini. 

Itaendelea Kesho.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: