Thursday, August 30, 2018

Maaskofu na wachungaji mkoani Mwanza wakubali kuisapoti Kwaneema Radio 98.1 Mhz.Fabian Fanuel @FMG
MWANZA.

Watumishi wa Mungu Maaskofu na Wachungaji kutoka katika jiji la Mwanza ambapo inapatikana radio Kwaneema Fm 98.1 wamekubali kuisapoti radio hiyo kutimiza maono yake makubwa ya kuujenga ufalme ya Mungu hapa Mwanza na Mikoa mingine.

Wameyasema hayo katika kikao baina ya uongozi wa Radio Kwaneema FM na Watumishi  hao wa Mungu kilichofanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Westland iliyoko Kiloleli wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Radio Kwaneema FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Radio hiyo Mailande Mpemba amesema anawashukuru watumishi wa Mungu kutoka jijini Mwanza kwa kuiunga mkono Radio na maono yake, kwa kurusha matangazo na vipindi vyao katika radio hiyo.

Amesema wanafarijika kwa miaka yote minane wamefanya kazi kubwa na watumishi wa Mungu kutoka madhehebu mbalimbali ya Mungu jijini Mwanza na nje ya hapo kwa uzuri na kuomba ushirikiano huo uendelee kuwa mkubwa ili kusapoti maono hayo yatimize malengo yake.

Akizungumza kwa niaba ya Bodi ya wadhamini wa Radio, Kiongozi wa Bodi hiyo Pasta Pius Rwegasila kutoka kanisa la Tanzania Field Evengelism TFE amesema anashukuru kwa mwitikio wa watumishi wa Mungu kufika katika kikao hicho na huo utakuwa utaratibu wa kila mwaka kukutana na watumishi hao kuzungumzia utendaji wa kazi hiyo.

Kwa niaba ya Wachungaji na Maaskofu, Askofu Joyce Mangu kutoka kanisa la Calvary Mwanza na Mchungaji Aron Lubango wamesem huo ni mwanzo mpya wa kuifanya kazi ya Mungu kwa nguvu katika kuisapoti radio hiyo na kutoa rai kwa watumishi wote wa Mungu kuunga mkono umoja huo ambao umeasisiwa leo.

Kwaneema Fm Radio imeanza tarehe kumi na moja mwezi wa tatu mwaka elfu mbili na kumi na hadi sasa imetimiza miaka minane katika utendaji wake ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mnara wake unaogharimu milioni sabini na tano tu. 

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: