Sunday, August 19, 2018

Ligi Pendwa ya Uingereza Man city Moto hauzimi ni mwendo wa kutoa dozi tuLigi pendwa ya uingereza imeendelea leo kwa michezo mitatu kupigwa na hadi sasa michezo miwili imekamilika  Man city wakishindwa 6-1 huku Watford wakishinda 3-1 dhidi ya Burnely.

Katika Mchezo wa Man city dhidi ya Huddersfield Town, city ikishinda Magoli 6-1 magoli ya washindi yamefungwa na Sergio Aguero aliyefunga magoli matatu dk ya 25,35 na 75 na kutimiza hat tricks 9 za ligi ya uingereza na kushika nafasi ya pili kwa kuwa na hat tricks nyingi na anazidiwa na Alan Shearer mwenye hat tricks 11.

magoli mengine yamefungwa na Gabriel Jesus dk 31 David Silva dk 48 na goli jingine wakijifunga kupitia kwa kongolo dk 84.

Mchezo mwingine magoli ya Andre Gray dk 3,Troy Deeney dk 48 na Will Hughes yametosha kuwapa ushindi Watford ya magoli 3 dhidi ya lile moja la Burnley lililofungwa na Tarkowski dk ya 6 tu ya mchezo.

Mchezo mwingine unapigwa saa kumi na mbili jioni ya leo ambapo Man United wakiwa ugenini dhidi ya Brighton and Hove Alibion na hapo kesho saa nne usiku majogoo wa jiji Liverpool wataumana na Crystal Palace.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: