Sunday, August 19, 2018

KYOMBO huyooo Afrika kusini, Mamelodi wamuhitaji bondeni kwa siku 10Mshambuliaji wa zamani wa Mbao Fc ya Mwanza ambaye hivi sasa ni mali halali ya Singida united Habibu Haji Kyombo ameitwa na timu ya Mamelodi Sundown ya Afrika kusini kwa ajili ya majaribio ya siku 10.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa klabu hiyo Festo Richard Sanga amethibitisha kuwa Kyombo ameshawasili Afrika ya kusini kwa ajili ya majaribio hayo na akifanikiwa ataanza rasmi kuitumikia timu hiyo na kuanza maisha ya soka la kulipwa nje ya nchi.

Uongozi wa klabu hiyo ya wakamua alizeti kupitia kwa mkurugenzi huyo wamesema wao wanamuombea afanikiwe na kutoa fursa kwa wadau wanaofwatilia soka la vijana kutia maguu pale singida kupata vijana wanaojua kucheza soka.

Amesema kuwa mbali na mahusiano yao mazuri na Mamelodi Sundown ya Afrika kusini pia wanamahusiano mema pia na Kaizer Chiefs zote za Afrika ya kusini.

Habib Kyombo ni mchezaji wa timu ya taifa ya Taifa Stars na anakumbukwa kwa kuifunga Yanga magoli mawili mwishoni mwa mwaka jana kwenye ushindi wa 2-0 akiwa na waajiri wake wa zamani klabu ya Mbao FC ya Mwanza


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: