Sunday, August 26, 2018

Kwa watu wazima tu...Sifa za kiongozi bora hizi hapa...


Na Pastor Zakayo Nzogele

1. ANATUMIA "MASIKIO" YAKE ZAIDI YA "MDOMO" WAKE: Kiongozi awe mwepesi wa kusikia mambo lakini awe mwangalifu katika kuongea.

2. KUTUNZA SIRI/MAAZIMIO YA VIKAO VYA UONGOZI: Kiongozi ASIYEFAA ni yule anayetoa SIRI za vikao kwa lengo la KUMUUMIZA Kiongozi au kuuhujumu uongozi uliopo (ambao na yeye ni sehemu ya uongozi) na kutaka KUJIONYESHA kuwa yeye ni wa tofauti na wengine.

3. KUTOTANGULIZA CHUKI AU HISIA BINAFSI KATIKA MAAMUZI: Kiongozi ni lazima aheshimu utu wa kila mtu hata ambaye haelewani naye. Kiongozi awe MTENDA HAKI kwa wote.

4. KAZI KUBWA YA KIONGOZI NI KUBORESHA MAISHA YA WATU... SIYO KUYAHARIBU: Hata walio-dhaifu bado Kiongozi anao wajibu wa kuwasaidia kwa UPENDO na SUBIRA.

NB: KIONGOZI; USIMUUMIZE MTU KWA MAKUSUDI KWA KUTUMIA NAFASI YAKO, MANENO AU MATENDO YAKO!!

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: