Friday, August 24, 2018

Kiungo hatari wa Simba anayekubalika na Manara aitwa ZambiaKiungo wa Simba, anayekubalika na Afisa habari wa Mnyama Haji Manara,Clatous Chama amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 26 wa Zambia ‘Chipolopolo’ kinachojiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Namibia.
Chama ameonyesha uwezo mkubwa katika mechi za kirafiki akiwa na mabingwa hao wa Tanzania tangu akiwa kambini Uturuki na hata aliporejea nchini bado alikuwa moto.
Kiungo huyo ambaye alijiunga na Simba Julai mwaka huu akitokea Dynamo ya Zambia ni miongoni mwa majina 26 ya wachezaji wa Zambia ambao watakaocheza na Namibia, Septemba 11 katika mchezo huo.
Bado Chama hajaanza kuichezea Simba katika mechi za mashindano kutokana na hati yake ya kimataifa ya usajili (ITC) kutokutumwa mpaka sasa yeye pamoja na Golikipa Deo Munishi.
Mbali na Chama nyota wengine wa Simba walioitwa kwenye timu zao za taifa ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco wote Tanzania, Emmanuel Okwi na Juuko Murshid (Uganda), Haruna Niyonzima na Meddie Kagere (Rwanda).SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: