Thursday, August 23, 2018

Kama mlivyosikia Makambovic Amjibu Kagere Yanga ikiichapa Mtibwa sugar
Mshambuliaji Heritier Makambo amefunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa Taifa.
Matokeo hayo yamewafanya yanga kujikita nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara TPL ikiwa na alama 3 sawa na timu nyingine sita zilizoshinda michezo yake ya awali.
Makambo amefunga goli lake la kwanza la ligi na kwanza kwa Yanga msimu huu  dakika ya 31 baada ya kupokea krosi nzuri  uliopigwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael.
Nahodha Kelvin Yondani aliifungia Yanga bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 40 kufuatia Mrisho Ngasa kufanyiwa madhambi na beki wa mtibwa sugar Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ndani ya 18.
Kipindi cha pili Mtibwa ilirudi kwa kasi kutaka kusawazisha bao hilo huku kocha Zuberi Katwila akifanya mabadiliko ya haraka ambayo yaliongeza nguvu kikosini.
Haruna Chanongo ndiye aliyeipatia Mtibwa goli la kufutia machozi baada ya kuingia  kuchukua nafasi ya Salum Kihimbwa na kufunga goli hilo dakika ya 72 baada ya piga nikupige katika lango la Yanga.
Jitihada za Mlinda mlango wa Yanga Beno Kakolanya zimewafanya yanga kuibuka na ushindi baada ya kuokoa michomo ya kutosha katika mchezo huo.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: