Friday, August 24, 2018

Idara ya kiungo Kuamua ubingwa wa EPL 2018-2019.

Na Jumanne-Eden Ally

Ligi kuu ya England ndio hiyo imeanza rasmi tarehe 10 August kwa mabingwa wa kihistoria, Manchester United wakicheza dhidi ya mabingwa wa msimu wa 2015/16 Leicester City na United wakishinda 2-1. Mabingwa mwaka 2016/17, Chelsea wakiwa ugenini dhidi ya Huddersfield Town wakishinda 3-0. Spurs wakiwa wageni dhidi ya Newcastle United nao wakashinda 2-1. Huku timu zilizosajili sana Wolverhampton na Everton zikitoka sare ya 2-2. 

Leo hii mabingwa wa zamani wa miaka ya 90 ikiwa inaitwa ligi daraja la kwanza, Liverpool watakuwa na Westham united huku Arsenal mabingwa wa mwaka 2003/04 watakaribisha mabingwa watetezi,Manchester city .

Ligi hii miaka kadhaa imekuwa na mabadiliko ya kiushindani na sasa kuna Top 6 kutoka Top 4. 
Timu za Chelsea na Arsenal zina kocha na meneja mpya huku Man United, Man city, Spurs na Liverpool zikiwa na meneja walewale.

Vilabu hivi vimepata maingizo mapya hususani katika idara muhimu ya kiungo ukabaji, uchezeshaji ili kuleta uwiano bora katika vikosi vyao katika kuzuia na kushambulia kutokana na mifumo husika kama 3-5-2(spurs, chelsea,man city, man united), 4-2-3-1/ 4-3-2-1(Chelsea,Liverpool, Arsenal,man united, man city,spurs), 4-4-2(Chelsea, Arsenal,spurs), 4-3-3(man united, Liverpool, man city, spurs). 

Mifumo hii yote itaenda sambamba na aina ya michezo na ubora wa timu pinzani kama kumiliki (possession), kushambulia kwa kasi baada ya kupokonya mpira (breakthrough ), Mchezo wa kasi( High tempo), au mchezo wa kujilinda zaidi (Defensive game). 

Kuna wachezaji kadhaa wameingia katika vikosi hivi ili kuongeza ubora zaidi na kuvihimalisha vikosi hivi ikiwa sajili za wachezaji kadha kama Fred, Jorginho, kovacic, Mahrez, fabinho, keita,Torreirra. 

Hii inapelekea kutengeneza muunganiko mpya katika safu zao ingawa spurs na citizens wao watabakia kama awali kutokana na kutokuwa na ingizo katika eneo hilo. 

◾Arsenal itakuwa na Torreirra/ Ramsey/ Ozil au Xhaka/Torreirra/ Ozil, Henrikh.

◾Chelsea itakuwa na Kante/Jorginho/ kovacic au kante/ Jorginho/ Fabregas au kante/ fabregas/ kovacic.

◾Man city itakuwa na Fernandinho/ De Bruyen/Silva au Fernandinho/KDB/ Gundogan na Ferdinandinho/ B.Silva/ Gundogan

◾Man united itakuwa na Matic/Pogba/ Fred au Matic/Perreira/ Pogba au Herreira/Perreira/Pogba au herreira/Fred/ pogba.

◾liverpool itakuwa na fabinho/ Henderson/ keita au keita/milner/ Henderson au Henderson/ keita/ Shaqiri na milner/ georgino/ keita

◾Spurs itakuwa na Dembele/ Eriksen/Alli au wanyama/ dembele/ alli au Wanyama/ eriksen/ Alli au Dembele/Wanyama/ Eriksen.

🌠Timu ipi itagharishwa kwa kiungo wake kufanya vyema zaidi msimu huu!?
Tayari Liverpool imetuma ujumbe, Chelsea imetuliza mzuka, United na Spurs wanavizia,


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: