Friday, August 17, 2018

Habari picha Simba ilivyotua kibabe mwanza kuwakabili mtibwa kesho kirumba


Kikosi cha Simba kikitua Mwanza tayari kwa mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mashabiki wa Simba wakiwa wanapita kwenye barabara ya Kenyatta Road Jijini Mwanza wakielekea Uwanja wa ndenge wa Mwanza kuipokea timu ya Simba kuekekea mchezo wao dhidi ya Mtibwa kwenye Ngao ya hisani.

Kocha mpya wa timu ya Simba Patrick Aussems akiongea na waandishi wa habari kuekekea mchezo wao wa Ngao ya hisani kesho CCM Kirumba dhidi ya Mtibwa, kushoto ni Naodha wa Simba John Bocco na kulia ni kocha wa timu ya Mtibwa Zuber Katwila.

Simba imetua Mwanza leo kutokea Arusha walikokuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha united walioshinda 2-1 na wapinzani wao klabu ya mtibwa ilitua usiku wa jana tayari kwa mchezo huo wa ngao ya hisani kesho uwanja wa CCM Kirumba saa kumi kamili jioni.
SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: