Friday, August 24, 2018

Fursa ziliyotolewa na Ubalozi wa India- RC Mwanza

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akifungua mkutano baina ya balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza uliolenga kuangazia fursa za kibiashara kati ya Mwanza na India.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka wafanyabiashara kutumia vyema fursa za kibiashara zilizofunguliwa na Ubalozi wa India hapa nchini kwa kutanua wigo wa biashara zao.

Mhe. Mongella ametoa rai hiyo wakati akifungua mkutano baina ya Balozi wa India nchini Tanzania na wafanyabiashara mkoani Mwanza kupitia taasisi ya wafanyabiashara wa kilimo na viwanda TCCIA uliofanyika jana katika ukumbi wa Rock City Mall Jijini Mwanza.

Alisema Tanzania na India ni nchi ambazo zina uhusiano wa miaka mingi tangu enzi za Uhuru hivyo wawekezaji na wafanyabiashara mkoani Mwanza watumie fursa iliyotolewa na India ya kuwaunganisha na wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hiyo hatua itakayoleta chachu ya mafanikio katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Awali Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya alisema nchi hiyo ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa nchini Tanzania ikiwa na uwezo wa hali ya juu katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali hususani zana kilimo, viwanda, vyombo vya usafiri, afya pamoja na elimu hivyo mkutano huo umelenga kuongeza ushirikiano zaidi wa kibiashara baina ya India na Tanzania.

Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari alieleza fursa mbalimbali zilizopo mkoani Mwanza ikiwemo uwekezaji wa viwanda vya nguo, bidhaa za ngozi, ujenzi wa makazi ya kisasa pamoja na ufugaji wa samaki na hivyo kuhimiza India kutumia vyema fursa hizo kuwekeza mkoani Mwanza huku watanzania nao wakitumia fursa ya ushirikiano uliopo na India kwenda kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya akielezea fursa za kibiashara zilizopo India na namna India inashirikiana na Tanzania kibiashara
Katibu wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Hassan Karambi akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Mshiriki akichangia mada
Mshiriki
Wanafunzi pia walialikwa kwenye mkutano huo ili kujifunza fursa za kibiashara baina ya Mwanza na India
Mshiriki akichangia mada
Mgeni rasmi, RC John Mongella akiwasili ukumbini
Mgeni rasmi akikagua mabanda ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa India
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto), akiagana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Sandeep Arya (kulia).

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: