Sunday, August 26, 2018

Chelsea,Watford kama Liverpool zashinda michezo mitatu hadi sasa United kesho na spursLigi kuu nchini uingereza imeendelea hii leo kwa michezo mitatu kupigwa kunako viwanja vitatu tofauti ambapo Watford walikuwa wanawaalika Crystal palace,Fulham wakaumana na Burnley na mchezo wa mwisho Chelsea the blues dhidi ya Newcastle united.

Chelsea wao wameshinda mchezo wa tatu mfululizo kama ilivyo kwa Livepool na Watford baada ya kupata ushindi wa magoli  2-1 dhidi ya Newcastle united goli la penalti la Eden Hazard dk 76 na Jingine wapinzania wakijifunga dk ya 87.

Watford wameichapa Crystal palace magoli 2-1 huku Roberto pereyra wa Watford akifunga goli moja dk 53 na goli lake la 3 kwenye ligi hadi sasa na goli jingine likifungwa na jose holebs dk 71, Crystal palace wakifutia machozi goli la Wilfred zaha dk 78.

Fulham wamepata ushindi wao wa kwanza hii leo baada ya kuwafunga Burnley goli 4-2 katika mchezo huo.

Ligi hiyo pendwa ya uingereza itaendelea kesho kwa mchezo mmoja ambapo Manchester United watakipiga na Tottenham majira ya saa nne kamili usiku.


SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: