Tuesday, August 28, 2018

Askofu Mkuu kanisa la EAGT Tanzania Dr Brown Mwakipesile kuwafunda watumishi wa Mungu Kanda ya Ziwa.

Mwandishi Wetu @FMG
MWANZA.

Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Tanzania Dr Brown Mwakipesile ataendesha semina kwa watumishi wa Mungu kutoka Kanda ya Ziwa kutoka Makanisa ya EAGT na Makanisa mengine katika Ukumbi wa Chuo cha waalimu Butimba kuanzia jumatano tarehe ishirini na nane agosti na alhamis tarehe ishirini na tisa agosti mwaka huu ili kuwapa mbinu na maelekezo ya kuchunga kanisa la Mungu.

Akizungumza na Blogu ya Famara News Askofu wa Kanisa la EAGT Kanda ya Ziwa Pasta George Gecha alisema kuwa itakuwa na semina kubwa na ya aina yake maana maandalizi yako vizuri na kila ,mtumishi amekwisha kupewa taarifa na mwaliko kushiriki katika semina hiyo kubwa ambayo itakwenda kuleta mabadiliko chanya katika utumishi wao.

Sambamba na Askofu Mkuu Dr Mwakipesile kufundisha katika semina hiyo, pia atakuwepo Katibu Mkuu wa Kanisa la EAGT Tanzania Dr Leonard Mwizarubi wakishirikiana vyema na viongozi wa kanisa la EAGT Kanda ya Ziwa.

Washiriki wa Semina hiyo ni maaskofu wote, wachungaji, waalimu, wainjilisti, wakurugenzi wa idara, wazee wa kanisa, mashemashi, viongozi wa idara kutoka makanisani na kiongozi yoyote kutoka nje ya kanisa la EAGT ambaye anataka kuongeza Elimu katika utumishi shambani mwa Mungu.

Jana Askofu Mkuu wa EAGT Tanzania Dr Mwakipesile alizindua kanisa la Eagt Buswelu linaloongozwa na Pasta Paul Mkonga. Kanisa hilo mwanzoni lilikuwa eneo la Pasiansi ila kwa sasa limehamia Buswelu baada ya kujengwa eneo hilo kutokana na kanisa hilo kuwa dogo huko lilipokuwa Pasiansi.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: