Saturday, August 25, 2018

Arsenal mambo safi Majogoo wa Jiji Liverpool mwendo mdundo
Klabu ya majogoo wa jiji Liverpool wameshinda mchezo wao wa 23 bila kupoteza katika uwanja wao wa nyumbani baada ya kuichapa Brighton goli 1-0.
Goli la Liverpool limefungwa na mfungaji bora wa msimu uliopita Mohamed salah dk ya 23 na kuipa Liverpool ushindi wa 3 mfululizo.
Livepool ndo timu pekee nchini uingereza ambayo haijafungwa goli hata moja hadi sasa wakiwa wamefunga magoli 7 kwenye mechi 3.
Mchezo mwingine Timu ya washika mitutu wa London Arsenal imepata ushindi wa kwanza katika ligi kuu Uingereza baada ya kuwafunga wagonga nyundo  West Ham United mabao 3-1 kwenye uwanja wa Emirates.
Arsenal ilipoteza michezo miwili iliyopita dhidi ya Manchester City na Liverpool hivyo ni ushindi wa kwanza wa kocha Unai Emery.
West Ham ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 25 kupitia kwa Marko Arnautovic baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Filipe Anderson.
Mlinzi Nacho Monreal aliisawazishia Arsenal bao hilo dakika ya 30 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa ‘Hammers’.
Mlinzi Issa Diop alijifunga dakika ya 70 katika jitihada za kuokoa mpira wa Alexander Lacazzate huku Danny Welbeck akimalizia la mwisho dakika za nyongeza kipindi cha pili.SHARE THIS

Author:

Facebook Comment

0 comments: