Tuesday, August 28, 2018

Ajiua kwa kujirusha kutoka juu ya Ghorofa Hospital ya Bugando Mwanza.Fabian Fanuel @FMG
MWANZA.

Mwanamke mmoja mtawa aitwaye Suzana Bathlomeo, miaka 48, Mkurugenzi wa Mipango na Fedha wa Hospital ya Rufaa ya Bugando, amefariki dunia baada ya kujirusha toka ghorofa ya pili ya hosptali ya rufaa ya bugando na kudondoka chini.

Mtawa huyo amefariki dunia asubuhi ya leo ya wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo, na kupelekea kuumia  maeneo ya kiuno na mgongo, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa, hata hivyo uchunguzi wa awali unaonesha kuwa katika ofisi aliyokuwa akiifanyia kazi  marehemu ambapo yeye alikuwa kiongozi zipo tuhuma za upovu wa fedha zaidi ya milioni mia tatu, ambazo zilipelekea baadhi ya watumishi wenzake kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi na wengine kufukuzwa kazi.

Aidha polisi bado wapo katika upelelezi kuhusiana na tukio hilo, huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi wa Polisi Jonathan Shana anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapoona wamekwenda kinyume na taratibu za kazi kama vile kujitoa uhai au kujijeruhi kwani ni kosa kisheri.

Sambamba na hilo anawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: