Tuesday, July 17, 2018

YANGA YAGOMEA USAFIRI NA HOTELI NCHINI KENYA

Klabu ya Yanga ambayo inatarajia kucheza mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia Jumatano hii, imegomea usafiri waliondaliwa pamoja na hoteli mara baada ya kutua nchini humo.

Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo iliandaliwa usafiri wa basi kutoka uwanjani hadi hotelini lakini ikaukataa na badala yake ikakodi usafiri wao na walipofika hotelini waligoma kuingia ndani ya hoteli hiyo bila kutoa sababu yoyote kulingana na maelezo ya katibu wa Gor Mahia, Ben Omondi.

"Tabia hii imekuwa ni kawaida kwa klabu za Afrika lakini nataka kuwahakikishia Yanga kuwa sisi hatujawahi na hatutoshiriki katika masuala ya kishirikina hata mara moja" Amesema Omondi.

Nikukumbushe tu kuwa katika michuano ya CECAFA Kagame Cup, Klabu ya Gor Mahia nao waligomea chumba cha kubadilishia nguo walichokuwa wameandaliwa na badala yake walitumia korido kubadilishia nguo huku wakidai kuwa Azam FC kupuliza dawa katika chumba hicho.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: