Tuesday, July 24, 2018

WAZIRI MHAGAMA AISAMBARATISHA BODI YA WADHAMINI NSSF

Waziri wa Nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama ameivunja bodi ya wadhamini wa shirika la Taifa wa hifadhi ya Jamii (NSSF).

Jenista ametangaza kutengeua uteuzi wote wa bodi kuanzia leo na kusema kwamba utaratibu wa uteuzi wa bodi mpya unafanyika.

Mhagama amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuhakikisha shirika linaimarishwa katika kusimamia mwenendo wa kila siku wa shirika ikiwemo kazi ya msingi ya kuongeza wanachama kukusanya michango pamoja na kulipa mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi kwa uzalendo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: