Tuesday, July 31, 2018

WAZIRI LUGOLA AMPA ZITTO SIKU MBILI KURIPOTI POLISI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kujisalimisha kwa mkuu wa polisi mkoani Lindi ili achukuliwe hatua stahiki kwa kuongea maneno ya uchochezi kwenye jimbo la Kilwa alipoalikwa na Mbunge Seleman Bungara maarufu Bwege.

"Kosa jingine la Zitto nikwenda kufanya mkutano eneo ambalo sio la kwake kwa mujibu wa taratibu. Nampa siku mbili ajisalimishe kwa RPC (Kamanda wa polisi Mkoa wa Lindi)", amesema Lugola.

"Akikaidi nitamuagiza IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro) amkamate popote alipo. Nishasema na nitaendelea kusema katika uchuguzi huu na chaguzi zijazo watu wanaotukana viongozi hawatabaki salama"amesema.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: