Tuesday, July 31, 2018

WATUMISHI 3 WATUMBULIWA KAZI KWA TUHUMA ZA WIZI WA DAWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu wa hospitali ya wilaya ya Kasulu kutokana na tuhuma za wizi wa dawa katika hospitali hiyo.

Baada ya kutembelea hospitali hiyo amesema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na malamiko ya wizi wa dawa na vifaa vya hospitali, wizi huo unaofanywa na watumishi wasio waaminifu wanaoiba vitu vya hospitali na kuuza maduka ya nje ambapo Waziri ameagiza kuundwa kwa tume ya kuchunguza suala hilo.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa kwa sasa wanatoa asilimia 85 ya dawa zinazohitajika nchini ili kusaidia wagonjwa kupata huduma, ambapo amesema serikali haitasita kumchukulia hatua mtumishi atakayekuwa na tabia ya wizi na kutojali kazi yake.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: