Tuesday, July 31, 2018

Wananchi washutushwa na Ongezeko la Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.Wakati takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi jijini Mwanza ikizidi kuongezeka wakazi wa jiji la mwanza wamekumbwa na taharuki juu ya takwimu za ugonjwa huo.

Akizungumzia hali diwani wa kata ya Ibungilo iliyopo wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Yusuph Msoke  amesema kuwa idadi kubwa ya watu wa Mwanza hawajui afya zao hususani watu wanaoishi maeneo ya visiwani hali inayoashiria kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya ukumwi.

Kwa upande wao wanaume Mkoani hapo wameiomba serikali kutoa elimu visiwani na maeneo mengine ambayo sio rafiki kwako kwani kuna baadhi ya watu wanaogopa kujua afya zao huku wakihofia wakuta wameathirika na virusi vya ukimwi.

Maambukizi ya VVU Mkoani Mwanza yameongezeka kutoka asilimia 4.2 ya miaka miwili iliyopita hadi kufikia asilimia 7.2 mwaka huu,huku Wilaya ya Sengerema,Nyamagana na Maeneo ya uvuvi yakitajwa kuwa ni makundi yanayojihusisha na biashara za ngono.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: