Monday, July 16, 2018

WANAKIJIJI WALIPIZA KISASI KWA KUUA MAMBA 300

Wanakijiji wa kijiji kimoja huko Indonesia wameua takribani mamba 300 baada ya mwanakijiji mwenzao kutafunwa na mmoja wa mamba hao na kufariki.

Tukio hilo limetokea katika jimno la Papua ambapo, mwanakijiji Sagito (48) alitumbukia katika bwawa linalotunza mamba hao wakati akitafuta majani yakulishia mifugo yake.

Wanakijiji hao walikasirishwa na uwepo wa bwawa hilo karibu na makazi ya watu ndipo walipoelekea kituo cha Polisi kutoa taarifa lakini licha ya mmiliki wa bwawa kukubali kulipa fidia, wananchi hao hawakuweza kukubaliana na uamuzi wake na kuamua kuwauwa mamba hao.

Mamlaka ya Polisi nchini humo imekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wapo katika uchunguzi baada ya kukamilika itafungua mashitaka kwa wahusika wa mauwaji hayo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: