Tuesday, July 31, 2018

Neema yaja kwa Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri Mkoani Mwanza.LUCY SANKA,
MWANZA.

Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji [Daladala] katika jiji la Mwanza wametakiwa kusajili vyombo vyao chini ya makampuni au mashirika ambayo yamesajiliwa na Serikali ilikupunguza ajali za barabarani.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa Hassan Dede wakati akizungumza na Famara News mapema leo ofisini kwake.

Amesema usajili huu wa kampuni umeshaanza kwa baadhi ya wamiliki na kuwataka ambao hawajajiunga katika makampuni hayo wachukue muda huu kufanya hivyo ili kufanya kazi kwa faida zaidi.

Aidha Hassan Dede amesema kuwa yeye akiwa mwenyekiti wa chama cha madereva kanda ya ziwa mfumo huo unakuja ikiwa ni katika kuunga mkono rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli.

Hata hivyo amewashauri madereva wazingatie sheria za barabarani na wajiandae kwa mabadiliko ya mfumo wa kazi zao kwani sasa watakuwa wanalipwa mishahara kama wafanyakazi wengine.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: