Monday, July 23, 2018

WAFANYA BIASHARA WALIA NA BEI YA CHUMVI

Wafanya biashara wa Chumvi katika Mkoa wa Mtwara wamesema pamoja na Serikali kutoa madini joto bure yanayochanganywa kwenye chumvi.

Wapo watu baadhi wamekuwa wakiwauzia bidhaa hiyo kwa bei ya shilingi Elfu sabini kwa kilo na hivyo kufanya baadhi ya watengenezaji wa chumvi kushindwa kumudu gharama na kujikuta chumvi nyingi kuingia sokoni biila kuwa na madini joto.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha watengeneza Chumvi Mkoa wa Mtwara, Bwana Festo Balegele ambaye amesema kukosekana kwa madini joto katika chumvi kunahathari kubwa kwa watoto wadogo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: