Tuesday, July 31, 2018

WADAU MWANZA WAISHAURI PAMBA SC.


NA ABDALLAH CHAUS
MWANZA
Wadau wa soka Jijini hapa wametoa maoni yao kwa viongozi wa timu ya Pamba sc inayojiandaa na kushiriki katika ligi daraja la kwanza msimu ujao 2018/2019,kuhakikisha wanafanya usajili wenye tija katika timu hiyo ili kurejesha ushindani katika soka la Mwanza kama zamani.
Wakizungumza na Famara News kwa nyakati tofauti wadau hao walisema,wanatamani kuiona Pamba kama ya Miaka ya nyuma,ambayo ilikua na ushindani katika soka la Tanzania hata kufanikiwa kucheza katika michuano ya kimataifa.
‘’Tumekua tunashangaa sana kuona timu yetu ya Pamba haifanyi vizuri katika michezo yake ya ligi faraja la kwanza na kuonekana kila msimu wako palepale na hakuna wanachofanya,tuna usihi na kuomba ufanye usajili wakutisha na Pamba sc irejee katika soka kama zamani””walisema wadau hao.
Hatahivyo wadau hao hawakusita kueleza masikitiko yao juu ya viongozi wa timu hiyo,kutokana na kuwa kimya mpaka sasa licha ya kumtangaza Kocha Hassan Banyai kama Kocha mkuu wa klabu hiyo,huku wakiweka wazi kua wanatakiwa kubadilisha mfumo wao wa kuiendesha timu hiyo.
Pamba sc maarufu kama TP Lindanda ilitangaza kuingia kandarasi ya miaka miwili na aliyewahi kua kocha mkuu wa klabu ya Njombe mji fc,huku ikiwa imejipanga usajili wa wachezaji wapya katika msimu ujao kutokana wachezaji wake wote kumaliza mikataba yao mara tu ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza msimu uliopita.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: