Tuesday, July 17, 2018

VIDEO YA MARAFIKI WA DUNIA YAKE JANETH KONJE KUACHIWA USIKU HUU YOUTUBE..

Fabian Fanuel, Mwanza.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza JANETH KONJE leo 17/7/2018 Saa 6 Usiku ataachia Wimbo wake uitwao Marafiki wa Dunia YouTube.
Akizungumza na Gospel 255 na Famara News Janeth amesema ameamua kuachia Wimbo huo baada ya kuushuti kwa kiwango Kikubwa na ubora chini yake Director Vippers kutoka Motions Pictures.
Amesema baada ya Ukimia wa Muda Kuandaa chakula kizuri Sasa ana Furaha kuwa amefanya Kitu ambacho kitawagusa watu wote, " Namshukuru Mungu kwa hatua hii nilipofikia kushuti Video yangu Marafiki wa Dunia, haikuwa kazi rahisi Ila Mungu amenipa kibali na neema kufikia hatua hii".
Amewaomba mashabiki wake kutembelea akaunti yake YouTube wasubscribe ili Wimbo huo utakapowekwa leo usiku wawe wa kwanza kuupokea na pia wasisite kumsapoti na kumwombea..

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: