Thursday, July 5, 2018

Timu ya Elininyo kutoka Ilala yainyuka Washiriki Vijibweni goli nne kwa bila.Christina Mwagala

TIMU ya Elininyo kutoka Ilala,jana imewashikisha adabu wenyeji wa mchezo kombe la Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Washariki kwa kuwa adabisha magoli manne kwa sifuri.

Magoli ya Elininyo yaliwekwa wavuni kupitiwa kwa wachezaji wake Yohana Mkomola ambaye alifunga magoli mawili kwa dakika 16 kipindi cha pili na dakika 40 kipindi hicho cha pili.

Aidha magoli mengine yaliwekwa kimyani na chezaji wao, James Kaimba dakika ya 36 na dakika sita ya kipindi cha pili.
Maulidi Mpaeka ,ambaye ni katibu wa Timu ya Washari alisema kwamba kutokana na kupoteza kwa mchezo huo uliopigwa jana katika kiunga cha Mzimu,wamepoteza matumaini ya kuingia hatua ya robo fainali.

Alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na kwamba walipata nafasi lakini walishindwa kuzitumia na hivyo kufanya wapinzani wao kuibuka mshindi.

“Wenzetu wamepata nafasi wamezitumia vizuri, tulijiandaa ila wenzetu walijiandaa zaidi yetu, lakini kwa matokeo ya leo hatuna uhakika wa kuingia robo fainali, tumecheza michezo mitatu,tumetoka sare mmoja, tumefungwa miwili” alisema Mpaeka.

Kwaupande wake Mwalimu wa Timu ya Elininyo,Malik Charles alisema kuwa siri ya ushindi huo ni kutokana na kupanga vijana wengi ambao wanacheza michezo tofauti tofauti ya uchezaji.
Alisema kuwa walipanga  viungo wegi jambo ambalo aliamini kuwa linaweza kuwapatia ushindi wa haraka kama ambavyo imejitokeza na kushinda goli nne kwa sifuri.

“ Hadi sasa nimejihakikishia kuingia kwenye hatua ya robo fainali,nitapanga kikosi kizuri zaidi, kipindi cha kwanza kuna makosa mengi ambayo tuliyafanya na hivyo kushindwa kupata goli,ila tulirudi na kusawazisha ndio mana tumepata ushindi mnono” alisema.
Hata hivyo,ligi hiyo bado inaendelea ambapo leo Timu ya Majukumu itakutana na timu ya Msoto zote za Vijibweni zitamenyana katika uwanja huo wa Mzimu.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: