Monday, July 16, 2018

SIWEZI KUONDOKA CCM NINA HISA - NAPE

Mbunge wa Mtama kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amesema kuwa hawezi kukiacha chama hicho tawala kwa sababu ana hisa nyingi sana.

Nape ametoa kauli hiyo jana jioni Jumapili Julai 15,2018 alipokuwa akizungumza na Wanachi wa Mtama Mkoani Lindi katika Mkutano wa hadhara.

Nape amewasihi wanachi hao kuondoa hofu juu yake akiwataka kupuuza maneno yanayosemwa kuhusu hatima yake yakubaki CCM, na kusisitiza kuwa hawezi kuondoka katika chama hicho.

"Nina hisa nyingi najua mmenielewa furaha yangu nikuwatumikia lakini hayo mengine ni bla bla tu" Amesema Nape.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: