Tuesday, July 24, 2018

SIMBA YAPEWA SIKU 75 NA TFF IFANYE UCHAGUZI MKUU

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ameitaka klabu ya Simba kufanya uchaguzi wao ndani ya siku 75.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirikisho hilo amesema kwamba kamati ya uchaguzi imemfikishia taarifa kuwa Simba wanatakiwa kufanya uchaguzi wao Mkuu.

"Kawaida huwa ni siku 60 na ndivyo ninavyojua mimi, lakini kamati ya uchaguzi imewapa siku 75 nazani siku 15 ni zamaandalizi, wanatakiwa wafanye uchaguzi wao mzima ili waweze kupata viongozi wao" Amesema Karia.

Klabu ya Simba kwa sasa ipo nchini Uturuki wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Bara.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: