Friday, July 6, 2018

SIMBA TAIFA KUBWA, KUNANI? ZILE 20B ZA MO MMEPEWA AU BADO?

Na Mandala J.

Jamani tunahitaji kuona  timu yetu hii ikisonga mbele kimaendeleo kwa uwekezaji murua tuliokubaliana nao. Lakini katiba yenu inaonesha uongozi uliopo madarakani umeisha toka tarehe 29/06 mko kimya mnataka nini mnataka mgogoro kumkatisha tamaa muwekezaji wetu mlioamua kumpa timu au ? Na timu ikose utulivu wa kufanya maendeleo.

Jamani tunahitaji mabadiliko makubwa sana tena ya kusonga mbele pamoja na kuachana na mambo yalioturudisha nyuma miaka nenda rudi kama hili na tukumbuke muwekezaji hupenda kuweka pesa yake katika sehemu tulivu.

Badilikeni Simba, Simba mbona tunaimba mabadiliko lakini matendo yaleyale.

Maana tuna maswali ya kuwauliza nyie viongozi japokuwa mtakosa legal status ya kujibu na kwa chochote mtakachofanya kwa kuanzia 29/06 kitakuwa hakina legal status hili ni kosa au hamuoni na kina athari kubwa sana leo na kesho.

Naona ndio maana hata muwekezaji zile 20bn kashindwa kuwapa anajua kifuatacho ITV ni Tamthilia ya kusisimua ya Isindigo( The need ) kama kule tumelipa hamjalipa leteni objectivity evidence nao hawana patamu sana haaa haaa haaa haaa mi sikuwa mhasibu ni kweli.
Au ndio mnasubiri hizo pesa iwe kama issue ya Emmanuel Okwi ya dollar 319 mpaka Leo hatujui ziko wapi? Na jumba mbovu wameshushiwa wale ile kamati ilikuwa haihusiki kweli? Duuh hii ndio nchi mkuu wa kaya anahangaika nayo acha tumuombe aangazie na huku na nina uhakika ataangazia tu ni suala la muda tu .

Na hata 20% ya mauzo ya Samatta kwenda Genk yako wapi? Si mlisema hivyoo tutapata hizo percentage, tumuulize nani maana mmekosa Integrity toka kwenye suala la pesa za Emmanuel Okwi.

Kiukweli kama waziri huku katika mpira kuna madudu mno  jamani viongozi wa vilabu hivi katika maswali muhimu hawana majibu kabisa na tumechoka.

Ondokeni kwa utaratibu ili Simba isije kurudi nyuma kwa migogoro isio na tija, na sie tusinyamaze,  mnaona tunaongea ila nia yetu ni kuona Simba isirudi nyuma kimaendeleo na iwe ndio timu ya mfano na funzo kwa vilabu vingine na hasa Yanga.

Mo usitoe hizo pesa mpaka wasepe japo duuh mpaka Leo kutokutoa hizo billioni huku timu unaihudumia kuna swali hapo au hoja au ni  kama ile ya Manji ya kukopeshana na ushawakata deni lako mkuu.

Sisi sisi jamani sijui tumerogwa na nani?

Mi nawakumbusha na kumbukeni wajibu wenu na nafsi zetu ziseme inatosha kuna watu wanaumia sana.

Ahsanteni.

+255659797279
+255620639779

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: