Wednesday, July 11, 2018

SIMBA SC USO KWA USO NA AZAM FC FAINALI KOMBE LA KAGAME CUP

Klabu ya Wekendu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kuingia fainali ya Kombe la KAGAME CUP baada ya kuichalaza timu ya JKU ya Zanzibar bao 1-0, bao ambalo limefungwa dakika 44 na mshambuliajia mpya wa Simba Meddie Kagere na kuwafanya Wekundu hao wa Msimbazi kutinga Fainali.

Simba SC sasa watakutana na Azam FC katika fainali ya Kombe hilo la Kagame CUP, ambapo Azam nao wameingia fainali baada ya Kuiduwaza timu ya Gor Mahia, huku michezo yote ya Nusu fainali ikiwa imechezwa katika Dimba la Taifa leo Julai 11, 2018.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: