Monday, July 9, 2018

SERIKALI YASAINI MIKATABA YENYE GHARAMA YA BILIONI 11.9

Wizara ya Madini imesaini mikataba mitatu na kampuni ya SUMA JKT ya mradi wa ujenzi wa vituo vya umahiri saba pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika Chuo cha Madini Dodoma inayogharimu zaidi ya shilingi Bilioni kumi na moja na Milioni miatisa.

Waziri wa Madini Mhe. Angella Kairiki amesema ujenzi wa miradi hiyo inatekerezwa kupitia mradi wa usimamizi endelevu wa rasilimali kwa lengo la kuboresha manufaa ya sekta ya madini hasa kwa wachimbaji wadogo ili kuwaongezea ujuzi na kukuza uchumi.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo Mkurugenzi mwendeshaji kampuni ya ujenzi SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi amesema SUMA JKT imejipanga kukamilisha majengo hayo kwa muda wa miezi sita kupitia kanda zake mbalimbali ili kuboresha sekta hasa kwa wachimbaji wadogo.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: