Monday, July 30, 2018

SERIKALI KUKARABATI MELI ZINGINE KWA AJILI YA USAFIRISHAJI KATIKA ZIWA VICTORIA. LUCY SANKA, MWANZA

Serikali inatarajia kujenga meli mpya ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200,itakayokuwa inafanya safari zake kati ya Mwanza na Mkoa Wa Kagera.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi  Isack Kamwelwe  katika halfa ya upokeaji wa Kivuko kipya kitakachofanya safari zake Kati ya Kigongo Na Busisi Jijini Mwanza.

Waziri Kamwele amesema kuwa Serikali iko katika hatua ya Kukarabati Meli zilizoko katika Ziwa Victoria ili kurahisisha Usafirishaji wa Bidhaa mbalimbali katika Ziwa hilo.

Katika hatua nyingine Kamwele amesema kuwa  lengo la Serikali ni kuhimarisha Miundo mbinu Muhimu kwa ajili ya shuguli za kiuchumi ambapo Hivi  sasa Serikali inatarajia  kukarabati Meli mbalimbali zilizoko katika Ziwa Victoria.

Akiwa Jijini Mwanza Mhandisi Kamwele  amepokea Kivuko kipya Cha Kigongo-Busisi ambacho kimegalimu kiasi cha takribani Bilioni 8.9.

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: