Monday, July 9, 2018

RONALDO KUWEKA HADHARANI MAISHA YAKE HALISI KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

Mchezaji nyota wa timu ya Taifa ya Ureno ambaye pia anakipiga katika klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepata dili nono kupitia mtandao wa Facebook, ambapo Ronaldo na familia yake wataanda Reality Show.

Kwa mujibu wa mtandao wa Variety umeeleza kuwa Facebook wapo kwenye mazungumzo na Ronaldo kuhusu kipindi hicho ambapo imeelezwa tayari wametenga dau la dola Milioni $ 10 ambayo nisawa na Tsh Bilioni 22 za kumlipa mchezaji huyo wa dunia.

Kipindi hicho kitahusu maisha halisi ya Ronaldo ndani na nje ya uwanja huku na mchumba wake Georgina Rodriguez na familia yake itahusishwa kwenye Reality Show hiyo.

Reality Show hiyo itakuwa na Episode 13 na itaoneshwa kupitia mtandao wa Facebook kwenye sehemu ya Facebook Watch, mpaka sasa bado haiwekwa wazi siku itakayo anza Reality Show hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wake pamoja na wapenzi wote wa soka.


SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: