Tuesday, July 17, 2018

RONALDO AWEKA REKODI JUVENTUS NDANI YA MASAA 24 PEKEE

Nyota wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo siku ya jana amefanikiwa kuweka rekodi nyingine katika klabu yake mpya ya Juventus ambayo siku ya jana ndio ilimtambulisha rasmi nyota huyo.

Katika utambulisho huo uliotanguliwa na vipimo vya afya ambao ulifanyika Jumatatu ya Julai 16, Ronaldo aliweka historia katika klabu hiyo ya kuwa mchezaji aliyeuza jezi nyingi kwa siku moja baada ya klabu kuuza jezi 520,000 ambazo ziliingiza kiasi cha dolla Milioni 60 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 136.

Kwa idadi hiyo ya jezi ya Ronaldo iliyouzwa ni pungufu ya jezi 330,000 kufikia idadi ya mauzo ya jezi ya msimu mzima wa 2016/17 ya klabu ya Juve.

Katika utambulisho huo Ronaldo alipata nafasi ya kuzungumza na katika mazungumzo hayo Nyota huyo amesema kuwa "Naajiona niko imara kwangu hii ni changamoto nyingine, Ligi ningumu lakini kwa kuwa Juventus wako tayari, na mimi nitakuwa tayari. Umri wangu si kitu muhimu  najisikia vizuri na niko tayari kwa kuanza kazi"

SHARE THIS

Facebook Comment

0 comments: